Hivi kweli mnatarajia nini kutoka kwa ´Amr Khaalid?


Swali: Tunapenda kujua ´Amr Khaalid ni nani na khaswa kwa kuzingatia ya kwamba watu wa vijiji vingi vilivyoko jirani wanampenda na wanamfuata kwa kuwa wanaonelea kuwa ni mlinganizi katika Uislamu.

Jibu: ´Amr Khaalid hazingatiwi ni katika wanachuoni. Ni mtu wa kawaida. Amesomea Uingereza. Nadhani bado alikuwa akichukua shahada yake ya udaktari huko Uingereza. Ni mtu wa kawaida. Sio katika wanachuoni ambao zinaaminiwa elimu na fataawaa zao.

Ni mtu wa kawaida, wa kisasa. Yeye mwenyewe anahitajia wanachuoni watakaomfunza na kumwelekeza. Ananyoa ndevu na anavaa suruwali na tai. Anachanganyika na wanawake ajinabi waliovaa vibaya kwa njia ya kuonyesha mapambo. Ni mtu masikini, ni mtu wa kawaida. Hastahiki jambo jipya. Ni mtu wa kawaida. Ana makosa mengi. Kwa sababu ya ujinga wa baadhi ya watu hawatofautishi kati ya mwanachuoni na mjinga na kati ya mwanachuoni na mchawi. Kama mnavyojua baadhi ya watu wa vijijini wengine wanakuwa wachawi. Pamoja na hivyo kuna wenye kumfuata. Ana kilemba, kanzu na anawaongoza watu katika swalah. Hata hivyo wanajua kuwa ni mchawi na anaandika herizi. Pamoja na hivyo wanamfuata. Ni vipi wanaswali nyuma ya mchawi, kuhani na mwanajimu? Haya ni kutokana na ujinga wa baadhi ya watu. Hawawezi kutofautisha kati ya mwanachuoni na mchawi na kati ya mwanachuoni na mjinga. Isipokuwa tu wale waliorehemewa na Allaah.

Mambo ni kama mlivyosikia ni mtu wa kawaida. Yeye anahitajia elimu zaidi kuliko nyinyi mnavyohitajia. Nyinyi mmeachia ndevu na mmevaa vizuri na mna kilemba na kanzu. Lakini yeye sivyo hivyo. Amenyoa ndevu. Amevaa tai na suruwali na anachanganyika na wanawake. Amepinda. Anahitajia wanachuoni wa kumfunza na anahitajia kufanyiwa upole.

Kuhusiana na kwamba amesomea Uingereza, mtu anatakiwa kutambua kwamba kusomea katika miji ya kikafiri sio jambo la kuaminika na khaswa masomo ya kiislamu. Ikiwa mwalimu wake wa kwanza ni mnaswara, wapili ni myahudi, watatu msitashiriki na mwanasekula na wanne mmasoni – unatarajia mwanafunzi atakuwa vipi ilihali daktari ni wa sampuli hii? Tunamuomba Allaah uimara juu ya Qur-aan na Sunnah. Kwa mwerevu inatosha kuashiria.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Wasswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.darulhadith.com/v2/vad-forvantar-ni-er-av-%C2%B4amr-khalid-egentligen/
  • Imechapishwa: 10/04/2017