Historia ya Mtume (صلى الله عليه وسلم) haisomwi mfungo sita peke yake

Swali: Hii leo kumekithiri mazungumzo katika magazeti, TV na Khutbah za ijumaa misikitini kuhusu historia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), haki zake na tabia zake kwa sababu ya kukaribia siku ya kuzaliwa kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni ipi hukumu ya kitendo hichi? Una nasaha zipi kwa Ummah juu ya jambo hilo?

Jibu: Ndio. Kusoma historia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), tabia zake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kukumbusha kumpenda na kumfuata ni jambo lililowekwa katika Shari´ah. Lakini hata hivyo haliwekewi siku maalum. Jambo hili linafanyika mwaka mzima. Kuhusu ambaye anachagua wakati huu na hazungumzi kuhusu historia wala kuhusu sifa za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) isipokuwa tu katika wakati huu, hii ni njia ya kuhuisha Bid´ah. Zindukeni juu ya hilo. Zindukeni juu ya hilo; kufanya siku maalum katika wakati huu ambao ni karibu na sehemu ya Bid´ah hiyo ina maana kwamba ni kushirikiana na wazushi juu ya kuhuisha Bid´ah. Hakuna kilichokufanya wewe kusoma historia ya Mtume katika wakati huu isipokuwa ni kwa sababu zitafufuliwa Bid´ah hizi punde tu. Hivyo wewe unakuwa ni mwenye kushirikiana nao na kuwapa nguvu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=25227
  • Imechapishwa: 02/11/2019