Hina au wanja wenye kudumu kwa muda mrefu ni sawa na kufanya chale?

Swali: Kati ya wanawake na khaswa kwenye masomo ya wasichana kumedhihiri kitu kinachoitwa ´wanja wenye kukamata`. Ni wanja unaodumu kwa wakati mrefu. Je, hilo linaingia katika hukumu ya kupiga chale? Ni zipi nasaha zako kwa wanawake katika hilo?

Jibu: Hilo haliingii katika kupiga chale. Kwa sababu chale ni ule wanja au rangi inaingizwa ndani ya ngozi na haifutiki kabisa. Ama wanja huu unafutika. Lakini mimi napenda kuwazindua watu juu ya nyenzo hizi kama vile wanja wenye kudumu kwa muda mrefu, nywele bandia na mfano wa hayo. Vitu kama hivi hapana shaka kwamba vina nyenzo za kemikali. Kuathiri ngozi ya mtu ni jambo lisilopingika. Lakini madhara hayo hayaonekani kwa mtu isipokuwa baada ya kupita muda. Kwa ajili hiyo natarajia kutoka kwa dada zetu na kutoka kwa ndugu zetu wazinduke juu ya nukta hii. Nyenzo hizi za kemikali ni jambo lisiloepukika kuwa na athari kwenye ngozi. Ama vitu vya kimaumbile kama vile wanja wa kawaida ni kitu kisichodhuru. Kwa hiyo tuzinduke juu ya kitu hichi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1323
  • Imechapishwa: 04/11/2019