Hili ndio lengo la Ahl-ul-Bid´ah kuweka Manhaj-ul-Muwaazanaah

Uko wapi uadilifu wanaodai. Wanasema kuwa pindi tunapotaja mabaya ya Ahl-ul-Bid´ah… Kwanza wao hawataki kabisa utaje mabaya ya Ahl-ul-Bid´ah. [Sauti haiko wazi]. Wameweka Manhaj-ul-Muwaazanaah ili kuwalinda Ahl-ul-Bid´ah. Wanaonelea pindi Salafiyyuun wanapomkosoa mmoja katika vingozi wao wanasema kuwa ni wajibu kutaja pia mazuri yao. Lakini wao wanapowashambulia na kuwatukana Ahl-us-Sunnah kwa matusi mbali mbali, hawatumii Manhaj-ul-Muwaazanaah hata kidogo na kwa hali yoyote ile. Manhaj-ul-Muwaazanaah hii wameiweka kwa kuwakusudia viongozi wa Bid´ah na upotevu na vitabu vya Bid´ah na upotevu. Matendo yao ni ushahidi mkubwa ya kwamba hawakuweka mfumo huu isipokuwa ni kwa sababu ya kutaka kuinusuru batili na Bid´ah na kuihami na kuwahami watu wake.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/HamadOthman/Divers/05Rabee01.mp3
  • Imechapishwa: 26/08/2020