Hijrah ni wajibu kwa muislamu ikiwa makafiri wamempa uhuru katika miji yao?

Swali: Leo katika baadhi ya miji ya kikafiri ambayo sio ya kiarabu waislamu wanakuwa na amani na hawaudhiwi. Waislamu wanatekeleza faradhi zao kwa uhuru mkamilifu. Je, ni wajibu kwa muislamu huko kufanya Hijrah kwenda katika mji wa waislamu?

Jibu: Ndio, ni wajibu kufanya Hijrah. Maadamu anaweza kufanya Hijrah ni wajibu kwake kufanya Hijrah. Aishi katika miji ya makafiri kwa kadiri ya dharurah. Dharurah ikiondoka ahame kwenda katika mji wa waislamu.

Sidhani kama anayeishi na makafiri ataachwa hivihivi. Hawawezi kumuacha na khaswa katika wakati huu kutokana na vitimbi vya mayahudi na manaswara leo uadui wao dhidi ya waislamu. Hawatomuacha. Lau watamuacha kwa muda fulani, basi hawatomuacha katika siku za mbele. Yuko khatarini na wao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (52) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-06-05.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014