Swali: Ni ipi hukumu ya kudumu kusema pale anapozikwa maiti:

“Muombeeni msamaha ndugu yenu na mumtakie uthabiti, kwani hakika hivi sasa atahojiwa”?

Jibu: Ndio, kila maiti wa Kiislamu anatakiwa kuambiwa hivi. Hivyo ndivyo alivyoamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kila maiti wa Kiislamu baada ya kumaliza kumzika wanatakiwa kusimama karibu na yeye na kumuombea uthabiti na msamaha. Muombeeni msamaha ndugu yenu na mumtakie uthabiti, kwani hakika hivi sasa atahojiwa. Hii ni Sunnah. Allaah (Jalla wa ´Alaa) alimkataza Mtume wake kusimama kwenye makaburi ya wanafiki:

وَلَا تُصَلِّ عَلَىٰ أَحَدٍ مِّنْهُم مَّاتَ أَبَدًا وَلَا تَقُمْ عَلَىٰ قَبْرِهِ

“Na wala usimswalie yeyote kamwe miongoni mwao akifa na wala usisimame kaburini kwake.” (09:84)

Bi maana kusimama baada ya kuzikwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17418
  • Imechapishwa: 10/12/2017