Hii ni hoja dhidi ya Qutbiyyuun


Swali: Wakati tunapowatajia upotevu wa Sayyid Qutwub Qutbiyyuun wanasema kwamba amejirejea katika upotevu wake. Je, unajua lolote kuhusu kujirejea kwa Sayyid Qutwub katika upotevu wake unaoenea?

Jibu: Hatujui lolote ya kwamba amejirejea katika upotevu wake na wala hakuandika lolote juu ya hilo.

Isitoshe hii ni hoja dhidi yao. Ikiwa kweli wanajua upotevu, kwa nini wanamfuata na kwa nini wanamtetea? Hii ni hoja dhidi yao.

Sisi tunajua kuwa Sayyid Qutwub amewakufurisha waislamu wote na amesema kuwa Uislamu ni [sauti haisikiki] na mambo mengine mengi ambayo yameasisiwa na hawa Hizbiyyuun Qutbiyyuun, Ikhwaaniyyuun, Albaniyyuun na Suruuriyyuun. Wote hawa wako juu ya utata huu. Wanamtetea Sayyid Qutwub ilihali wanajua fika ya kwamba yuko katika upotevu. Lakini haya ni matamanio ndio yanawafanya wakawa kama vipofu na viziwi. Tunamuomba Allaah afya na usalama.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alnajmi.net/voices.php?action=show&id=44
  • Imechapishwa: 05/09/2020