Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kusafiri kwa ajili ya dharurah kama kwenda katika Hajj na ´Umrah au nyinginezo bila ya kuwa na Mahram?

Jibu: Haijuzu kwa mwanamke kusafiri bila ya kuwa na Mahram. Sababu hizi alizotaja haisemwi kuwa ni dharurah. Hizi sio dharurah. Hata ikiwa ni Hajj harusiwi kusafiri bila ya kuwa na Mahram. Kwa ajili hii imethibiti katika Hadiyth Swahiyh ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri bila ya kuwa na Mahram.” Akasimama mwanaume mmoja na kusema: “Ewe Mtume wa Allaah, hakika mke wangu ameenda kwa ajili ya kuhiji na mimi nimeshasajiliwa kwenda katika vita kadhaa na kadhaa.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Rejea na uhiji pamoja na mwanamke wako.” Hadiyth hii ni Swahiyh.

Mwanaume huyu ameandikwa kwenda kupigana Jihaad na wakati alipomwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa mke wake ameenda kwenda kuhiji akamwamrisha kuacha kwenda katika Jihaad na afuatane na mke wake ili awe Mahram wake.

Kwa ajili hii wanachuoni wamesema miongoni mwa masharti ya kuwajibika kwa Hajj kwa mwanamke ni apate Mahram wa kusuhubiana naye katika safari ya Hajj. Ikiwa hakupata Mahram basi anaweza kuweka niaba ya ambaye atamhijia. Hii sio dharurah. Dharurah ni kama anasafiri kwa ajili ya kufanya Hijrah kutoka katika mji wa kikafiri. Hii ni dharurah. Dharurah nyingine ni kama anaenda katika matibabu na mfano wa hayo, hizi ndio dharurah. Ama kusafiri kwa ajili ya kwenda Hajj, hii sio dharurah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://ar.islamway.net/lesson/138827/%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A3%D8%A9-%D8%AD%D9%82%D9%88%D9%82-%D9%88%D9%88%D8%A7%D8%AC%D8%A8%D8%A7%D8%AA?ref=s-pop Toleo la: 12-02-2015
  • Imechapishwa: 24/09/2020