Swali: Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowauliza wake zake kuhusu chakula na akawa hakupata kitu, kisha akasema:

“Basi mimi nimefunga.”

Je, mtu anapata kufahamu kujuzu kutamka kwa nia? Ni ipi hukumu ya anayetumia dalili juu ya hili?

Jibu: Hapana. Huku sio kutamka nia. Haya ni maelezo. Anaeleza kuwa amefunga. Bi maana kuanzia hivi ni mwenye kufunga. Sio kwa njia ya kutamka nia. Hakusema “Basi nimenuia kufunga”.

Kwa ajili hiyo, ndio maana mtu akimtukana mwenzake au akataka kugombana naye, anasema “Mimi nimefunga”. Hii si kwa njia ya kuelezea nia. Huku ni kuelezea Swawm tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (17) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-03-14.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014