Swali: Mwenye kutafuta elimu na akajifunza Qur-aan na Sunnah kisha akarejea kwa familia yake akawafundisha, akalingania katika Dini ya Allaah na katika kumpwekesha Allaah. Je, mtu aina hii anafikia daraja ya Mujaahiduun siku ya Qiyaamah?
Jibu: Ndio, hii ni Jihaad. Hii ni aina katika Jihaad. Ni aina kubwa katika Jihaad. Kulingania watu, kuwafundisha na kueneza kheri. Hii nii katika aina kubwa ya Jihaad.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (38) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-01-06.mp3
- Imechapishwa: 15/11/2014