Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

29- Mu’aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Nilisema: “Ee Mtume! Nieleze kitendo ambacho kitanipelekea kuingia Peponi na kitanikinga na Moto… “

Hapa kuna mafunzo ya kuwa na adabu kwa wanachuoni. Kwa sababu Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh) ndiye mtu ambaye ni mjuzi zaidi wa Ummah huu wa ya halali na ya haramu. Mu´aadh ni katika wanachuoni. Hii ni dalili inayoonesha ya kuwa inatakiwa kwa mwanafunzi awe ni mwenye kupupia juu ya yale yenye kumkukurubisha na Pepo na kumuweka mbali na Moto.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 402
  • Imechapishwa: 13/05/2020