Hii ndio dawa kila baada ya kutenda dhambi

Swali: Matatizo yangu na malalamiko yangu namshtakia Allaah kisha kwako. Kuna mtu anatumbukia katika dhambi kubwa siku zote na anajaribu kufanya tawbah kwa ukweli na Ikhlaasw. Lakini pamoja na hivyo anarudi. Ni ipi dawa na ufumbuzi wa mtazamo wako?

Jibu: Dawa na ufumbuzi atubie kwa Allaah. Kila anapotenda dhambi atubu kwa Allaah. Allaah anamsamehe yule mwenye kutubia. Lakini baada ya kutubia anapaswa kujiepusha na sababu zinazopelekea katika maasi haya. Anatakiwa kujitenga nazo mbali ili aweze kusalimika na shari yazo. Vilevile amtake msaada Allaah (´Azza wa Jall) na amuombe Allaah daima amthibitishe kutubia. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ni mkarimu. Abashiri kwamba kila pale anapotenda dhambi na akaomba msamaha na akatubu tawbah ya kweli kabisa na huku Allaah akajua kuwa ni mkweli, basi Allaah anamsamehe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/872
  • Imechapishwa: 06/07/2018