Swali: Je, mkusanyiko (Jamaa´ah) imeshurutishwa mtu aende msikitini? Mtu akiswali na mke wake nyumbani inazingatiwa kuwa ni mkusanyiko?

Jibu: Mwanaume na mwanamke haizingaitiwi kuwa ni mkusanyiko. Lakini hata hivyo inajuzu kwa mwanamke akamfuata mwanaume na akaswali nyuma yake. Lakini hata hivyo haizingatiwi. Mkusanyiko inatakiwa isiwe chini ya wanaume wawili na zaidi.

Aidha mkusanyiko unakuwa msikitini. Haiwi nyumbani isipokuwa kwa udhuru. Ikiwa una msikiti na kunaswaliwa mkusanyiko ni wajibu kwako kwenda na kuswali na mkusanyiko wa mskitini. Ispokuwa ikiwa kama una udhuru wa maradhi au khofu hapo unaweza kuswali nyumbani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13980
  • Imechapishwa: 22/04/2018