Hifadhi pesa benki na usichukue pesa ya ziada

Swali: Mtu anaweza kuwa anapata mshahara katika benki miongoni mabenki ambapo akazitumia lakini hata hivyo kukabaki pesa kidogo. Je, inajuzu kwake kuacha pesa hizo au ni lazima azichukue na kwamba akiziacha basi anasaidia katika ribaa?

Jibu: Kwanza kabla ya kujibu swali hili tunauliza: je, kuweka pesa benki ni halali au hapana? Tunasema mtu akihitajia kuzihifadhi hakuna neno[1]. Kwa sababu benki haifanyi kazi kwa ribaa asilimia kwa mia. Wana kazi ambazo ni za ribaa na zisizokuwa za ribaa. Kwa hivyo mtu akihitajia kuhifadhi pesa benki hakuna neno. Lakini asichukue ribaa kabisa. Vovyote itakavyokuwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَذَرُوا مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ فَإِن لَّمْ تَفْعَلُوا فَأْذَنُوا بِحَرْبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ

 “Enyi walioamini! Mcheni Allaah na acheni yaliyobakia katika ribaa ikiwa kweli nyinyi ni waumini. Msipofanya, basi tangazeni vita kutoka kwa Allaah na Mtume wake na mkitubu basi mtapata rasilimali zenu – msidhulumu na wala msidhulumiwe.[1]

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/bora-hifadhi-pesa-mahali-ambapo-hazitumiwi-katika-ribaa/ 

[1] 02:278-279

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/824
  • Imechapishwa: 18/03/2018