Hedhi imerefuka kwa sababu ya dawa ya kuzuia mimba

Swali: Kuna mwanamke hedhi yake imerefuka kwa sababu ya dawa ya kuzuia mimba iliyoingizwa ndani. Matokeo yake akawa si mwenye kuswali kwa kipindi cha siku ishirini. Afanye nini?

Jibu: Hili ni kosa. Kila chenye kuzidi juu ya siku kumi na tano anatakiwa kukilipa. Kikomo cha muda wa hedhi ni siku kumi na tano  na uchache wake ni mchana mmoja na usiku wake. Muda wake wa kawaida ni siku sita mpaka saba. Hedhi haitoki nje ya muundo huu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (29)
  • Imechapishwa: 11/02/2022