Haya ndio matunda ya Jihaad katika njia ya Allaah

Ni jambo linalotambulika kwamba ambaye kodi inachukuliwa kutoka kwake halinganii katika ukafiri. Akiwa atalingania katika ukafiri mkataba wake unavunjika. Ni mwenye kujisalimisha chini ya hukumu ya Kiislamu na analipa kodi katika hali ya unyonge. Huyu ndiye anaachwa. Mtumzima, mtoto na mwanamke ambao ukafiri wao hauvuki kwenda kwa wengine. Kadhalika mtawa ambaye amejitenga na watu na kwenda katika masinagogi yao. Watu aina hii wanaachwa.

Hii ni dalili yenye kuonyesha kuwa dini ya Uislamu sio dini ya mauaji na umwagaji damu. Ni dini ya rehema na uadilifu. Inataka kuwaondosha watu kutoka katika giza kwenda katika nuru kwa ajili ya manufaa yao wao wenyewe. Ni manufaa kiasi gani yamepatikana kwa watu kupitia Jihaad? Wale waliosilimu kutoka katika makafiri kwa wale wasiokuwa waarabu wamesalimishwa na Allaah kutokamana na Moto. Wangeachwa wangelikuwa miongoni mwa watu wa Motoni. Wamesilimu, wakaufanya vizuri Uislamu wao na ndani yao Allaah akawatoa wanachuoni vigogo. Haya ndio matunda ya Jihaad katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall). Jihaad ndio nundu ya Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydatu al-Imaam-il-Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 120
  • Imechapishwa: 30/01/2020