Swali: Baadhi wanawaita wale wenye kushikamana barabara na Qur-aan na Sunnah kwa ufahamu wa Salaf wa Ummah kwamba ni wapotevu. Wanasema kuwa ni lazima maandiko yasomwe upya na kwa njia inayoendana na zama. Unasemaje juu ya hili?

Jibu: Hapa ndipo kuna kosa. Maandiko yasomwe upya – bi maana watu waache mfumo wa Salaf na wa Ummah wa Kiislamu. Kwa msemo mwingine ni kwamba mnatakiwa kuachana nayo na muanze upya. Haya ndio malengo yao. Ibadilisheni dini yenu, kwa msemo mwingine, anzeni na dini mpya na kateni mafungamano yenu na Salaf. Haya ndio malengo yao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/18073
  • Imechapishwa: 12/07/2019