Hawezi kufanyiwa operesheni mpaka atolewe mimba yenye miezi mitano

Swali: Kuna mwanamke alifanya ajali mgongoni mwake akiwa ni mjamzito katika mwezi wa tano. Madaktari wakamthibitishia kumfanyia operesheni mgongo wake na wakashurutisha kutoa kipomoko tumboni. Lakini hata hivyo mama akakataa. Wakasema kwamba yuko khatarini ya kupoza mwili au kufa kabisa ikiwa hicho kipomoko kitaendelea kubaki tumboni na wala hakufanya tena ile operesheni. Ni kipi anachotakiwa kufanya hivi sasa?

Jibu: Haijuzu kukitoa hicho kipomoko ikiwa kutolewa kwake kitakufa hata kama kutakhofiwa juu ya mama kupoza kwa mwili au kufa kabisa. Mmesikia hukumu? Baada ya kipomoko kupuliziwa roho haijuzu kukitoa kwa hali yoyote na vovyote itavyokuwa. Kwa nini? Kwa sababu ukikitoa utakuwa umeiua nafsi kwa makusudi. Kipomoko ni muumini. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا

“Na yeyote atakayemuua muumini makusudi, basi malipo yake ni Moto ni mwenye kudumishwa humo na Allaah atamghadhibikia na atamlaani na atamuandalia adhabu kuu.”[1]

Jengine ni kwamba iwapo tutakitoa tuna uhakika kuwa mama atasalimika? Hapana. Huenda operesheni hiyo ikawa ni sababu ya kufa. Katika hali hiyo tutakuwa tumefanya makatazo yenye kuyakiniwa ili kuzuia madhara yasiyokuwa na uhakika.

Jengine tukikibakiza hichi kipomoko na mama akafariki au akapoza mwili, je, sisi ndio tutakuwa tumesababisha kufa kwake au kupoza kwake? Hapana. Haya ni kutoka kwa Allaah na Allaah anakadiria ayatakayo. Vilevile hatuna uhakika kwamba akibaki atakufa. Mara nyingi madaktari wanathibitisha kwamba mwanamke kipomoko chake kikibaki tumboni atakufa na mambo hayawi hivo. Mimi namjua vyema mwanamke mwenye mimba ambaye madaktari walithibitisha kuwa kipomoko chake kina ulemavu na kwamba ni lazima kukiporomosha. Uthibitisho wa kidaktari. Lakini akatoka hali ya kuwa ni mrembo. Hii ni dalili inayofahamisha kuwa wanaweza kukosea. Kwa hali yoyote tukikadiria kuwa asilimia kwa mia kwamba akibaki tumboni mwake mama ataangamia na kipomoko hicho kitaangamia, basi tungelisema kuwa kuangamia kwake hakuko mikononi mwetu. Bali ni jambo liko kwa Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 04:93

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1641
  • Imechapishwa: 11/05/2020