Hawafungi kamwe, bali wao daima ni kupiga ubwabwa

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipoulizwa kuhusu kufunga kwake siku ya jumatatu akasema:

“Hiyo ni siku niliyozaliwa.”

Inakusudiwa jumatatu yoyote ya mwaka. Kuifunga siku hiyo itakuwa imependekezwa na imewekwa katika Shari´ah. Mwenye kutaka kujikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa funga basi miongoni mwa swawm bora anazoweza kujikurubisha nazo ni swawm ya jumatatu ambapo amezaliwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haihusiani na siku moja tu. Bali ni siku zote za mwaka. Mtu anatakiwa kupupia kufunga jumatatu na kadhalika alkhamisi, kama ilivyopokelewa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya fadhilah za kufunga jumatatu na alkhamisi. Mtu anatakiwa kupupia hilo.

Ni jambo linalojulikana kwamba washerehekeaji wa maulidi hawafungi siku ya jumatatu. Wanachofanya ni kuandaa chakula, wanakula na wanajiburudisha kwa chakula na hawana jambo la kufunga. Kile kitu ambacho ameelekeza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakifanyi. Wanafanya kitu ambacho hakikufanywa wala hakukielekeza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wala hakikufanywa na makhaliyfah wake waongofu, wala hakikufanywa na Maswahabah zake na wala Taabi´uun, wala waliokuja baada ya Taabi´uun. Bali ni kitu kilichozuliwa katika karne ya nne ya Hijriyyah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
  • Imechapishwa: 03/11/2019