Hawa ni zaidi ya wanyama


Swali: Vipi kuhusu ulipuaji na kuharibu?

Jibu: Haya hayafanywi na yeyote isipokuwa watu ambao wametoka katika utu na wakawa kama wanyama wakali. Hawa sio wanaume na sio wanaadamu. Akili zao zimefutwa na akili zao zimechafuka na wakawa ni njia kuangamiza katika jamii.

Mtu akipoteza akili na akapoteza imani basi mnyama anakuwa ni bora kuliko yeye. Hapana nguvu wala hila isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Hiki ni kitendo kibaya na kitendo kisichomstahikia mwanaadamu sembuse muislamu. Muislamu hakutoki kwake madhara juu ya watu. Muislamu anakuwa ni kifaa cha kheri, kulingania katika dini ya Allaah, kuamrisha mema na kukataza maovu kwa njia inayostahiki.

  • Mhusika: Imaam Swalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 14/11/2017