Hakuna yeyote anayeswali kuelekea Ka´bah, muumini na mtenda madhambi, Ahl-us-Sunnah na Ahl-us-Sunnah, hawakuafikiana juu ya muislamu yeyote kwamba ni mwenye furaha na mwenye kuokoka huko Aakhirah – isipokuwa Maswahabah peke yao. Wala hawakuafikiana juu ya muislamu yeyote kwamba ni mla khasara na mla maangamivu. Unajua tofauti ilioko juu ya Abu Bakr as-Swiddiyq, mtu wa kipekee wa Ummah, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy na Ibn-uz-Zubayr. Vivyo hivyo al-Hajjaaj, al-Ma´muun na Bishr al-Marriysiy. Kadhalika Ahmad bin Hanbal, ash-Shaafi´iy, al-Bukhaariy, an-Nasaa´iy na kadhalika wema mpaka hii leo. Hakuna imamu yeyote aliyekamilika katika wema isipokuwa atapatikana mjinga au mzushi anayemkaripia na kumdharau. Na hakuna kiongozi katika Bid´ah katika Jahmiyyah au Raafidhwah isipokuwa watapatikana watu wanaomsapoti, wanamtetea na wanaonelea maoni yao kuwa ni dini kutokana na matamanivu na ujinga. Kinachozingatiwa ni kile chenye kusemwa na jopo la wengi ambao wamesalimika kutokamana na matamanivu na ujinga na wamesifika na uchaji na elimu.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/344-345)
  • Imechapishwa: 01/11/2020