Swali: Unasemaje juu ya yule mwenye kusema kitabu “Nawaaqidh-ul-Islaam” na “Kashf-us-Shubuhaat” vinawafunza watu Takfiyr na kuwafanya kuwa na ujasiri juu ya hilo. Bora zaidi ni kutowafunza watu navyo.

Jibu: Sisi tuliwaambieni katikati ya darsa kwamba wako wanaosema kwamba ni kwa nini mnawafunza watu mambo haya na mnawafafanulia nayo? Wanasema kwamba watu ni waislamu na inatosheleza wakawa waislamu hata kama watafanya yakufanya. Haya ndio maneno yanayosema. Hawa ndio maadui wa Tawhiyd. Wanashirikisha katika Tawhiyd. Hawaitaki Tawhiyd. Hawataki kusema neno “Tawhiyd”. Haya ndio malengo yao. Lakini yatasomeshwa haya, yatakaririwa katika masomo na yatafafanuliwa misikitini ziguse mchanga pua zao. Hili ndilo la wajibu kwa wanachuoni. Ni wajibu kwa watu wajifunze jambo hili. Kwa sababu huu ndio msingi wa dini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 57-58
  • Imechapishwa: 05/08/2018