Hatuhitajii tafsiri mbovu za shahaadah za Hizbiyyuun

Swali: Je, ni sahihi kufasiri shahaadah ya kwamba maana yake ni:

“Hakuna mwenye haki ya kuhukumu isipokuwa Allaah”

“Hakuna mwenye haki ya kuhukumu wala kitu kingine isipokuwa kutoka kwa Allaah”

“Hakuna utawala kwa yeyote juu ya mwengine kwa sababu utawala wote ni wa Allaah”

“Hana mshirika katika uumbaji”?

Jibu: Maana ya “Laa ilaaha illa Allaah” imebainishwa na wanachuoni. Hatuhitajii tafsiri hizi za al-Haakimiyyah wala tafsiri za vipote hivi vya karibuni. Shahaadah maana yake ni hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Hii ndio maana ya “Laa ilaaha illa Allaah”. al-Haakimiyyah ni sehemu katika ´ibaadah. Sio tafsiri ya shahaadah. Ni sehemu katika tafsiri yake. al-Haakimiyyah inaingia katika ´ibaadah. Kuhukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah kunaingia katika ´ibaadah. Lakini sio maana yote ya “Laa ilaaha illa Allaah”. Laa ilaaha illa Allaah imekusanya ´ibaadah aina zote. Aina zote za ´ibaadah zinaingia katika “Laa ilaaha illa Allaah”. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi, hivyo basi niabuduni.”

Kwa hivyo maana ya “Laa ilaaha illa Allaah” ni hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=oMoaMLGx4k0
  • Imechapishwa: 09/12/2017