Imaam at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hatuingilii hayo [maandiko kuhusu sifa za Allaah] kwa kuyapindisha maana yake sahihi au kuleta maoni fulani kutokana na matamanio yetu.”

Hatufanyi hivo kama walivofanya Mu´tazilah. Wamefikiri kuonekana kwa Allaah kunalazimisha awe na kiwiliwili au awe ndani ya kitu au awe na kikomo. Wamesema lau tutathibitisha kuonekana kwa Allaah, basi hilo litalazimisha awepo upande fulani, awe na kikomo, awe na mwili na awe ndani ya kitu fulani. Walipoleta fikira kama hizi ndipo wakawa wamekanusha kuonekana kwa Allaah na wakapindisha maana yake sahihi na kusema kuwa makusudio ni “elimu.”[1]

Makusudio ni kwamba hatuingii katika kuulizia namna ili tusije kuleta fikira mbovu kama walivofanya Mu´tazilah na Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal wengine.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/radd-juu-ya-utata-wa-wenye-kupinga-kuonekana-kwa-allaah-aakhirah/

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda: Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah
  • Imechapishwa: 29/05/2022