Hataki kuwa na mawasiliano na baba yake


Swali: Nina dada ambaye anakataa kuwa na mawasiliano na baba yake kwa sababu hamuulizii na wala hamjali na kwamba alimwacha kwa kaka yake baada ya mama yao kufa, wakati ambapo alikuwa ni mwenye kumuhitaji. Ni zipi nasaha zako kwa dada huyu juu ya baba yake?

Jibu: Namnasihi atubu kwa Allaah na amtendee wema baba yake. Kufanya hivi ni kumuasi baba yake. Haki zake hazianguki hata kama alimfanyia vibaya. Haki zake hazianguki. Kwa hivyo ni wajibu kwake kumtendea wema na kumtunza vizuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (67) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah22-05-1438h.mp3
  • Imechapishwa: 18/10/2017