al-Bahrayniy ameyawekea taaliki maneno ya Shaykh-ul-Islaam na kusema:

“Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ametaja ya kwamba wakati imani inapotajwa peke yake, basi kunaingia Uislamu na matendo mema. Ni kwa nini basi Rabiy´ anayandosha matendo mema katika imani?”[1]

Ni lini, ee mwongo, nimeyaondosha matendo mema katika imani? Yathibitishe hayo kuanzia mwanzoni mwa kuzaliwa kwangu mpaka hii leo kupitia vitabu vyangu au kanda zangu. Napambana na wale wenye kuyaondosha matendo katika imani na wale wanaopinga kuwa matendo ni tawi na ukamilifu wa imani na pia wale wenye kuyaondosha matendo katika imani, kama  anavofanya al-Fawziy. Nimesema katika kanda ambayo umeitumia vibaya kwa ajili kunipiga vita kwa batili na kwa dhambi:

“Allaah amrehemu imamu huyu[2]. Amekusanya katika mlango huu dalili nyingi zinazopambanua maneno yake:

“Imani ni maneno na vitendo, inazidi na kupungua… “

Nimezungumzia imani, matendo na Irjaa´  ambayo ni sawa na kurasa sita. Kwenye dawrah hiyohiyo nimezungumzia imani na matendo, nikabainisha ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah, ´Aqiydah ya Khawaarij na ´Aqiydah ya Murji-ah na kubainisha kuwa inazidi na kushuka. Miongoni mwa niliyoyasema:

“Matendo ni msingi wa imani. Imani pasi na matendo inaweza kupotea, mtu anaweza kutoka katika Uislamu na kushuka kiasi cha kwamba kusibaki kitu isipokuwa sawa na uzito wa mduduchungu.”

Pamoja na haya yote anakuja Haddaadiy huyu mtenda dhambi na kunituhumu Irjaa´ na kusema:

“Ni kwa nini basi Rabiy´ anayandosha matendo mema katika imani?”

Ananisemea uwongo sana uwongo ambao pengine Raafidhwah wakaona haya kuusema. Je, mfano wa mtenda dhambi huyu ambaye anawapiga vita Ahl-us-Sunnah anaweza kuwa katika Ahl-us-Sunnah wakweli na wenye muruwa? Kamwe.

[1] al-Burkaan, uk. 26

[2] al-Bukhaariy.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 163-171
  • Imechapishwa: 19/09/2023