Swali: Ipi hukumu ya kuhudhuria mwanamke katika hafla za ndoa ambazo zina wanawake walio uchi?

Jibu: Hili ni munkari. Na hili limeenea sana leo katika mikusanyiko ya wanawake – sehemu za starehe, minasaba ya ndoa hususan wajane wanahudhuria na nguo mbaya, mpaka walio uchi wanahudhuria – A´udhubillaah. Na hakuna yeyote anaekataza; si walii wake, mama yake wala yeyote wala waliohudhuria. Bali wanafurahishwa na hilo. Huu ni munkari na khatari kubwa kwa Ummah. Na hili likitokea katika mikutano baina ya wanawake, yule ambaye anaweza kubadili hili anaweza kukataza wanawake, ni wajibu kwake kuhudhuria kwa ajili ya kukataza munkari. Ama yule asiyeweza hilo [kukataza munkari] haijuzu kwake kuhudhuria kwa kuwa asipate madhambi akawa ameshiriki. Kwa kuwa mwenye kuacha kukataza munkari naye anaweza hilo anakuwa ameshiriki kwa yaliyofanya. Usihudhurie.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/allmohadrat?page=4
  • Imechapishwa: 09/11/2014