Swali: Je, anapewa udhuru yule ambaye anawaomba mawalii na anawataka uokozi ilihali anaishi kati ya waislamu na huku anasikia Qur-aan na Sunnah?

Jibu: Hapewi udhuru. Kwa kuwa hoja imemsimamia. Yule ambaye yuko mbali na hakusikia kitu chochote na hakufikiwa na kitu ndiye ambaye anazingatiwa ni katika watu ambao hawakupata Mtume yeyote. Mtu kama huyu ni lazima abainishiwe. Kuhusu yule ambaye anaishi kati ya waislamu, anasikia idhaa za redio, anasikia mihadhara na maneno ya wanachuoni hoja imemsimamia. Kwa hivyo hapewi udhuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (62) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd14-07-%201438.mp3
  • Imechapishwa: 06/08/2017