Swali: Mimi ni imamu wa msikiti. Mara nyingi hujiwa na maswali ya kawaida. Niwanukulie fatwa za wanachuoni wa leo juu ya mambo yenye kutatiza au nifanye jambo lingine?

Jibu: Hapana, haitoshelezi kunukuu fatwa. Pengine ukawa hukufahamu vizuri fatwa. Unaweza kunukuu makosa. Huenda fatwa ikawa inahusiana na mnasaba maalum na wewe ukaiweka pasipokuwa mahaka pake. Lililo salama zaidi kwako ni kusema kuwa hujui na kuwaelekeza kwa wanachuoni.

Swali: Wakati mwingine huniuliza maswali ya ndoa na ninawanukulia fatwa za Ibn Baaz (Rahimahu Allaah)…

Jibu: Hapana! Maswali ya ndoa ni khatari! Usiwape fatwa yoyote ya Ibn Baaz. Huzifahamu na hufahamu ni siri na hali gani ilio nyuma yazo. Waelekeze mahakamani au katika baraza la fatwa. Usiwape fatwa yoyote. Waelekeze katika mahakama ya Kishari´ah au baraza la fatwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (34) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20-%201%20-%202%20-%201436.mp3