Swali: Ni ipi hukumu ya kusikiliza redio na mfano wake ikiwa kile unachosikiliza au unachotazama ndani yake hakuna kitu cha haramu?
Jibu: Hapana neno kusikiliza kile kinachorushwa hewani kutoka katika redio katika Qur-aan tukufu, Hadiyth zenye kufidisha na taarifa ya khabari muhimu. Vivyo hivyo hapana vibaya kwa yale yanayorekodiwa katika Qur-aan tukufu, Hadiyth yenye kufidisha, nasaha na mengineyo. Nawasihi kusikiliza idhaa ya Qur-aan na barnamiji “Nuur ´alaad-Darb” kutokana na ile faida kubwa inayopatikana humo.
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/490)
- Imechapishwa: 05/03/2021