Hapa utakuwa unaenda kinyume na staili ya jamii


Swali: Ikiwa desturi ya nchi ni kuvaa kanzu iliyo juu ya kongo mbili za miguu, inazingatiwa ni shuhra kuivaa katikati ya muundi wa mguu?

Jibu: Inahesabika ni katika shuhra kwenda kinyume na desturi ya nchi ilihali wao ni wenye kuafikiana na Sunnah. Watamfikiria vibaya, kumsemea kwa ubaya na kushangazwa naye. Mtu asiendi kinyume na jamii ambayo haijafanya jambo la haramu, bali ni wenye kuafikiana na Sunnah. Sunnah ni kuwa na vazi lililo juu ya tindi mbili za miguu. Ikiwa watu wote katika mji wanavaa mpaka katikati ya muundi wa mguu, na wewe fanya hivo. Ikiwa wanavaa mpaka kwenye kongo ya mguu, na wewe fanya hivo. Ikiwa wanavaa kati ya kongo ya mguu na muundi wa mguu, na wewe fanya hivo. Yote hayo ni Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (11) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/14466
  • Imechapishwa: 10/10/2017