Swali: Kuna mtu ameapa ilihali ni mwongo kwa ajili ya kusuluhisha?

Jibu: Inafaa kusema uongo kwa ajili ya kusuluhu kati ya watu. Imekuja katika “as-Swahiyh” ya Muslim:

“Sio mwongo yule mwenye kufikisha kwa lengo la kheri au akasema kheri.”

Imekuja katika Hadiyth nyingine tena:

“Uongo hauruhusiwi isipokuwa katika mambo matatu; kutengeneza kati ya watu, mazungumzo ya mtu na mkewe na mazungumzo ya mke kwa mumewe.”

Hapa ni pale ambapo lengo la mtu ni kutengeneza na jambo hilo lisipelekee katika madhara. Kwa mfano mtu akamwendea mwengine na kumwambia kuwa fulani anajutia alichokifanya na anatamani kukutana nawe na anapenda mwelewane, lakini hata hivyo mtu huyo hakumwambia kitu. Anamwendea yule mwingine na kumwambia alivomwambia yule wa kwanza. Mfano wa kitendo hichi hakina neno. Vivyo hivyo mazungumzo ya mtu na mkewe kwa mfano akamwambia kwamba atamnunulia vitu kadhaa na kadhaa kwa lengo asuluhishe kati ya mzozo walionao. Lakini hatakiwi kuapa. Kwa sababu kiapo kinapelekea yamini. Akijichunga ndio bora zaidi. Akihitajia kufanya hivo hakuna neno muda wa kuwa anakusudia kutengeneza kwa sharti kusipelekee katika madhara mengine.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14)
  • Imechapishwa: 30/05/2020