Hapa ndipo tutakaribisha bunge

Swali: Je, inafaa kwa vijana wenye msimamo kuingia bungeni?

Jibu: Je, huko ananukuliwa Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Au huko ananukuliwa Bush na wengineo?

Ikiwa ni Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio wananukuliwa huko basi linakaribishwa. Vinginevyo ni katika aina ya maneno yaliyoharamishwa kuhusu ujumbe wa Allaah. Haijuzu kushiriki ndani. Muumini anayefuata dini anatahadharishwa kuketi na Ahl-ul-Bid´ah na wapotofu. Tusemeje juu ya hawa ambao wanawafuata wamagharibi, Ulaya, USA, Uingereza na wengine na kuigiliza misingi na upotevu wao?

Shikamaneni na Kitabu cha Allaah, Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na njia ya Salaf na kundi lililonusuriwa:

فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَىٰ

”Pale ambapo utakufikia mwongozo Wangu, basi hatopotea na wala hatopata tabu, na atakayeupa ukumbusho Wangu mgongo, basi hakika atapata maisha ya dhiki na tutamfufua siku ya Qiyaamah hali ya kuwa kipofu.”[1]

[1] 20:123-124