Hapa ndipo rangi ya zambarau inakuwa hedhi

201- Nimemsikia baba yangu akisema: ´Aashah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Kila umanjano na uchafuchafu anauona mwanamke wakati wa ada yake ya mwezi ni katika ada yake mpaka pale atakapoona mtiririko mweupe.”

202- Baba yangu amenihadithia: Muhammad bin Ja´far ametuhadithia: Sa´iyd ametuhadithia, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Hafswah, kutoka kwa Umm´ Atwiyyah al-Answaariyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesema:

“Tulikuwa hatuzingatii umanjano na uchafu baada ya kutwaharika kuwa ni kitu.”[1]

[1] Abu Daawuud (307).

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad (1/143)
  • Imechapishwa: 14/04/2021