Hapa ndipo madhambi madogo yanageuka makubwa

Swali: Mtu kuendelea kufanya madhambi madogo yanageuka kuwa madhambi makubwa?

Jibu: Ndio. Baadhi ya wanachuoni wamesema kwamba mtu kuendelea kufanya madhambi madogo kunayageuza kuwa makubwa. Amesema (Ta´ala) kuhusu sifa za wa chaji:

وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ

“Wale pale wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao, humdhukuru Allaah wakaomba msamaha kwa madhambi yao. Na nani anayesamehe madhambi isipokuwa Allaah na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua.”[1]

[1] 03:135

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 22/09/2019