Hapa ndipo itajuzu kugawa mirathi kabla ya mtu kufa

Swali:  Je, inajuzu kwa baba kugawa mirathi kwa watoto wakati bado yuko hai kwa kukhofia watoto wa kiume wasije kuwanyika watoto wa kike mirathi yao?

Jibu: Hakuna neno kwa kufanya hivo. Lakini asiwape sawa sawa. Anatakiwa kufanya uadilifu kati yao:

لِلذَّكَرِ مِثْلُ حَظِّ الْأُنثَيَيْنِ

“Mwanamume atastahiki mfano wa fungu la wanawake wawili.” (04:11)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14819
  • Imechapishwa: 28/06/2020