Hapa ndipo itadharurika kwa mwanamke kusafiri bila Mahram

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kusafiri bila ya kuwa na Mahram kutokana na dharurah kubwa?

Jibu: Haijuzu kwake kusafiri pasina Mahram. Kutokana na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Asisafiri mwanamke isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Wamekubaliana al-Bukhaariy na Muslim kwa usahihi wake kutoka katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa).

Ama ikiwa ni kwa dharurah kama mwenye kufanya Hijrah kwa ajili ya Allaah anatoka katika mji wa kikafiri na kuhamia katika mji wa Kiislamu na akakosa Mahram, ahame pamoja na watu waaminifu wanaume na wanawake, hakuna neno. Ama dharurah kubaki katika sehemu kama anakhofia juu ya nafsi yake Zinaa au kuuawa, akahamia katika mji mwingine, kutokana na kukhofia kuuawa au uchafu [wa Zinaa] au dharurah zingine kubwa kama hizo ambazo hana njia nyingine ya kuiepuka, hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=12822
  • Imechapishwa: 03/05/2015