Hapa ndipo inatakiwa kunyanyua mikono


Swali: Inajuzu kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa katika Khutbah ya ijumaa?

Jibu: Khatwiyb akiomba du´aa ya kuomba mvua, basi yeye na walioko pale wanatakiwa kunyanyua mikono yao. Hivyo ndivyo alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah. Hili linahusiana na wakati wa kuomba du´aa katika Khutbah ya ijumaa. Vinginevyo haijuzu kunyanyua mikono katika Khutbah ya ijumaa. Wala haijuzu kwa walioko pale kunyanyua mikono yao. Hii ni Bid´ah. Wanatakiwa kukatazwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/de
  • Imechapishwa: 30/09/2017