Hapa ndipo inafaa kwa mwanamke kusafiri bila Mahram


Swali: Inajuzu kwa mwanamke kusafiri bila Mahram akiwa ni mwenye haja ya kufanya hivo?

Jibu: Haijuzu kwake kufanya hivo isipokuwa pamoja na Mahram:

“Si halali kwa mwanamke anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”[1]

Wanasema isipokuwa tu ikiwa kama mwanamke anahajiri. Akihitajia kuhajiri inafaa kwake kusafiri hata kama ni bila Mahram.

[1] al-Bukhaariy (1088) na Muslim (1338).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (66) http://alfawzan.af.org.sa/node/16524
  • Imechapishwa: 13/08/2017