Hapa ndipo elimu inakuwa yenye kunufaisha


Swali: Mimi nina maombi na swali. Maombi yangu ni kuniombea kwa Allaah anipe elimu yenye manufaa na matendo mema.

Jibu: Kwa nini wewe peke yako? Hebu wacha tuwaombee wanafunzi wote. Tunamuomba Allaah atuelimishe sote, atunufaishe na atunufaishe kuyatendea kazi yale tuliyojifunza. Uhakika wa mambo ni kwamba elimu inamnufaisha yule mwenye kuitendea kazi, na inamdhuru yule ambaye haitendei kazi. Kama ambavo matendo mema hayanufaishi bila ya elimu yenye manufaa, basi vivyo hivyo elimu yenye manufaa hainufaishi pasi na matendo mema. Ni lazima yapatikane yote mawili. Kwa hivyo tunamuomba Allaah aturuzuku elimu yenye manufaa na matendo mema.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (586)
  • Imechapishwa: 20/09/2020