Hapa ndio utajua kama Jamaa´at-ut-Tabliygh ni katika makundi 72 yaliyopotea

Swali: Je, Jamaa´at-ut-Tabliygh ni miongoni mwa yale makundi yaliyotajwa katika Hadiyth?

Jibu: Kama unataka kujua ni miongoni mwa yale makundi yaliyotajwa katika Hadiyth, basi wapime na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ´Aqiydah ya Maswahabah. Ikiwa wanaafikiana nao, basi wako katika haki. Wakiwa wanaenda nao kinyume, basi ni katika makundi yaliyopotea. Hii ndio mizani. Wapime kwa Qur-aan na Sunnah. Qur-aan na Sunnah ndio vinavyowahukumu kama wao ni katika makundi yaliyopotea au siyo. Yule anayefuata njia ya Qur-aan na Sunnah, basi anaingia katika lile kundi lililookoka. Yule anayekwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah, basi anaingia katika yale makundi yaliyopotea. Waite majina unavotaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alfawzan.ws/sites/default/files/lsm–14330124.MP3 Tarehe: 1433-01-24/2011-12-20
  • Imechapishwa: 29/05/2022