Hapa mume hawezi kufanya uadilifu


Swali: Je, ni wajibu kufanya uadilifu kati ya wake wawili inapokuja katika mapenzi?

Jibu: Hakuna yeyote awezae kufanya uadilifu kati ya wake wawili inapokuja katika mapenzi:

وَلَن تَسْتَطِيعُوا أَن تَعْدِلُوا بَيْنَ النِّسَاءِ وَلَوْ حَرَصْتُمْ

“Wala hamtoweza kufanya uadilifu kati ya wake japokuwa mtatupia.”[1]

Bi maana katika mapenzi. Mtu hawezi kufanya uadilifu katika hili. Lakini hata hivyo asimili kwa yule anayempenda juu ya wale wengine katika matumizi, mavazi na malazi. Katika haya anatakiwa kufanya uadilifu.

[1] 04:129

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 27/10/2017