Hapa kuna dalili kwamba yule asiyeswali sio kafiri?

Swali 18: Hadiyth isemayo:

“Peponi hakutoacha kuwepo nafasi mpaka Allaah aumbe viumbe wengine na awafanye kukaa humo.”

Je, hapa si kuna dalili kwamba yule asiyeswali hakufuru?

Jibu: Hivi ndivo wanavosema Ahl-us-Sunnah; Ataumba watu ambapo atawaingiza Peponi kutokana na fadhilah na rehema Zake. Hivo ndivo kasema Shaykh-ul-Islaam katika ”al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah”. Kuna baadhi ya wapokezi wamekosea ambapo wamesema:

“Motoni hakutoacha kuwepo nafasi mpaka Allaah aumbe viumbe wengine na awafanye kukaa humo.”

Hili ni kosa. Usahihi ni kwamba nafasi itabaki Peponi ambapo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ataumba watu na kuwaingiza Peponi kutokana na fadhilah Zake. Watu hawa hawajapatapo kufanya kheri yoyote maishani. Katika Hadiyth hakuna dalili juu ya maudhui ya kuacha swalah. Kwa sababu Hadiyth inazungumzia kitu kimoja na kuacha swalah ni kitu kingine. Kule kuumba Kwake watu ambao hawajapatapo kufanya kheri yoyote maishani ni kutokana na fadhilah Zake. Hawakupatapo kupewa jukumu la matendo yao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 35
  • Imechapishwa: 09/10/2018