Swali: Je, ni kweli kwamba Hanaabilah ndio Salafiyyuun peke yao?

Jibu: Maneno haya si sahihi. Wema waliotangulia ni Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) na wale waliofuata njia yao katika wanafunzi wa Maswahabah, wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah ambao ni Hanafiyyah, Maalikiyyah, Shaafi´iyyah, Hanaabilah na wengineo waliofuata haki na wakashikamana barabara na Qur-aan na Sunnah safi katika mlango wa Tawhiyd, majina na sifa za Allaah na katika mambo mengine yote ya dini. Tunamwomba Allaah atujaalie kuwa miongoni mwao na atuwafikishe waislamu wote – watawala na wananchi – katika kila ambacho kinahusiana na kushikamana na Qur-aan na Sunnah. Aidha tuhukumu kwayo na tuhukumiwe kwayo na kujihadhari na kila kinachokwenda kinyume navyo. Kwani hakika Yeye ni mtawala na muwezo wa hayo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/238)
  • Imechapishwa: 10/07/2021