Hali za ulimwengu wa Kiislamu hii leo

Swali: Tunataka utusikilizishe maneno mafupi kuhusu hali za ulimwengu wa Kiislamu hii leo?

Jibu: Siwezi kukueleza hilo. Kwa sababu hili linahitajia kuizunguka miji yote ya Kiislamu na nibaki katika kila serikali na nchi kwa muda wa miezi miwili au mitatu ili niweze kutambua hali zao sawa za vijiji na miji yao. Lakini kwa mujibu wa vile tunavosikia kupitia vyombo vya khabari ni kwamba watu wako katika fitina mbalimbali; mauaji, uharibifu na mengineyo. Mwenye kustahikiwa ni Allaah (´Azza wa Jall). Ajabu ni kuwa mauaji na uharibifu unaweza kuwa kati ya waislamu wao kwa wao, kama mnavosikia wenyewe. Kwa ajili hii tunamuomba Allaah (´Azza wa Jall) aweke katika kila nchi ya Kiislamu uongozi mwema wenye kuongoza kwa Qur-aan na Sunnah. Watu wakirudi katika Qur-aan na Sunnah watapata mafanikio na kufaulu duniani na Aakhirah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/836
  • Imechapishwa: 30/03/2018