Hali za mswaliji aliyechelewa pamoja na imamu wake katika sujudu ya kusahau

Swali: Naomba kuelezwa kwa ufupi kuhusu yule mchelewaji pindi imamu wake ataposahau na akasujudu kabla ya Salaam au baada yake, je, yule mchelewaji asujudu katika hali zote mbili baada ya kukamilisha swalah yake?

Jibu: Mchelewaji imamu wake akisujudu kabla ya Salamu  ni lazima kwake kumfuata. Kwa sababu haijuzu kwa mchelewaji kufarikiana na imamu isipokuwa atapotoa salamu.

Ama endapo atasujudu baada ya salamu, katika hali hii asimfuate. Pale imamu tu atapotoa salamu anatakiwa kusimama na akidhi yale yaliyompita. Atapokamilisha ndipo tunatakiwa kutazama; ikiwa alijiunga na imamu baada ya kusahau, basi yeye atasujudu baada ya salamu, na ikiwa imamu alisahau kabla yeye hajajiunga naye, basi hana haja ya kusujudu. Hii ndio hukumu inayomwandama mswaliji kwa imamu wake katika sujudu ya kusahau.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1589
  • Imechapishwa: 23/10/2018