Swali: Hema letu lilikuwa Muzdalifah. Ili niweze kubaki Minaa angalau nusu ya usiku nikaenda huko wakati wa masiku ya Tashriyq. Je, kitendo changu kinazingatiwa ni kuchupa mipaka na ni sahihi?

Jibu: Ni miongoni mwa mambo ya wajibu na sio kuchupa mipaka. Ikiwa unaweza kuingia Minaa na kulala huko, japokuwa ni kwa kukaa, basi ni lazima ufanye hivo. Kwa sababu kitendo hicho ni wajibu cha hajj na sio kuchupa mipaka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (22) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdatul-26-3-1435.mp3
  • Imechapishwa: 18/03/2020