Swali: Mwombaji msikitini akienda mbele ya waswaliji na akaanza kutaja haja na hali yake akatazwe kufanya hivo kwa kutumia hoja makatazo ya kuulizia kilichopotea? Jengine ni kwa sababu anawashughulisha wenye kuswali kufanya Adhkaar zao baada ya swalah.

Jibu: Haitakikani kumzuia. Lakini ashauriwe. Baada ya hapo hali yake ikitambulika kwamba si muhitaji na kwamba si mwenye kustahiki, huyu arudishwe na akatazwe. Akiwa ni muhitaji apewe. Vivyo hivyo apewe ikiwa hali yake haijulikani. Kwa sababu anaweza kuwa ni mwenye kuhitaji. Kuna hali tatu za mwombaji:

1- Mtu ajue kuwa si muhitaji. Mtu kama huyu ni lazima kumzuia na kumrudisha.

2- Mtu ajue kuwa ni muhitajia. Inatakiwa kumsaidia na kumwacha.

3- Usiijue hali yake kama ni mwenye kuhitajia au si mwenye kuhitajia. Huyu inatakiwa kumwacha. Kwa sababu anaweza kuwa ni muhitaji na hivyo apewe. Lakini asiwashughulishe waswaliji wakati wa kufanya Adhkaar. Bali aketi mahala pake na abainishe hali yake baada ya watu kumaliza kufanya Adhkaar.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (11) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191491#219817
  • Imechapishwa: 06/07/2019