Kutokana na hilo kunabainika juu ya kwamba kumtii mtawala kumefungamana na hali tatu:

1- Kwanza: Jambo ambalo ni wajibu kutokana na msingi wa Shari´ah. Katika hali hii kiongozi anatiiwa kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) kuamrisha hilo. Kutii hapa sio katika haki zake, bali anatiiwa kutokana na haki ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa kumtii kwa yale aliyowajibisha.

2- Pili: Kiongozi kuamrisha au kukataza jambo ambalo limeruhusiwa, jambo lenye Ijtihaad, lenye kuchukiza au mfano wa hayo. Katika hali hii anatiiwa ikiwa hii ni haki yake kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) amemjaalia kusikizwa na kutiiwa.

3- Tatu: Maamrisho yake yakawa katika maasi au kukataza jambo la wajibu. Katika hali hii hatiiwi kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) kutiiwa ni haki yenye kutangulizwa juu ya utiifu kwa wengine miongoni mwa wale ambao Allaah Amewajaalia haki. Kwa mfano kuwatii wazazi wawili, mke kumtii mume wake, kumtii kiongozi na kadhalika miongoni mwa watu ambao Allaah (Jalla wa ´Alaa) amewajaalia haki ya kusikizwa na kutiiwa. Hawa wanatiiwa kwa yasiyokuwa maasi, bi maana katika mambo yaliyokuja katika Shari´ah juu ya kwamba sio haramu.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 386-387
  • Imechapishwa: 13/05/2020