Hali mbili za kuwa pamoja na watenda maasi


Swali: Mimi ni kijana ambaye natoka nchi ya kando ambaye natafuta elimu. Nina marafiki ambao sio wenye kushikamana na dini; wanavuta sigara na wakati mwingine wanacheza mpira. Lakini hata hivyo wanaswali na wachache katika wao hawaswali. Lakini hata hivyo nakaa nao huenda nikawatengeneza. Wakati fulani napata fursa ya kuwapa mawaidha na kuwakumbusha. Hili linaweza kutokea katika siku moja au zaidi mpaka pale kunapopatikana fursa. Ni ipi hukumu ya kukaa nao wakati wote mpaka pale nitaposafiri kutoka katika nchi hii?

Jibu: Akupende Allaah ambaye umenipenda kwa ajili Yake na namuomba Allaah atufanye wote kuwa katika wapenzi na mawalii Wake. Kuhusu yale aliyotaja kubaki na marafiki ambao wanafanya baadhi ya maasi,  huyu anatakiwa kutazama. Ikiwa kubaki kwake kuna manufaa na wakajizuia kutokamana na maasi, hakuna neno. Vinginevyo itakuwa haijuzu kwake kubaki pamoja nao. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ

“Hakika amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aaayah za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Vinginevyo mtakuwa kama wao.”[1]

Bi maana mkikaa nao basi nyinyi mtakuwa kama wao.

[1] 04:140

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/822
  • Imechapishwa: 05/03/2018